05 Feb 2025 / 112 views
Tetesi za soka Ulaya

Manchester United huenda ikamnunua mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Christopher Nkunku, 27, kwa mkopo ikiwa Muingereza Marcus Rashford, 27, ataondoka katika klabu hiyo.

Bayer Leverkusen wamefanya mawasiliano na Manchester City kuhusu uhamisho wa mkopo wa kiungo wa kati wa England chini ya umri wa miaka 21 James McAtee, 22.

Kocha wa City Pep Guardiola hatamzuia Mctee iwapo anataka kujiunga na mabingwa hao wa Ujerumani.

Kiungo wa kati wa Argentina Emiliano Buendia, 28, yuko mbioni kujiunga na Leverkusen kutoka Aston Villa kwa mkopo.

Villa pia wako kwenye mazungumzo na mlinzi wa Villarreal mwenye umri wa miaka 27 na Argentina Juan Foyth. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Villa na Colombia Jhon Duran, 21, analengwa na klabu ya Saudi Arabia Al-Nassr kwa euro 100m wakati wanatafuta mshirika mpya wa Cristiano Ronaldo.

Wolves wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa Lens na Austria yenye thamani ya £16m Kevin Danso.

Liverpool na Chelsea wako tayari kuchuana na Napoli kwa ajili ya kumnunua fowadi wa Borussia Dortmund na Ujerumani Karim Adeyemi, 23, lakini wanaweza kusubiri hadi msimu wa joto kufanya uhamisho.

Real Madrid, Bayern Munich na Juventus wanavutiwa na beki wa kimataifa wa Bournemouth chini ya umri wa miaka 21 Dean Huijsen.

Newcastle wanavutiwa na mlinzi wa kimataifa wa Ukraine wa Cherries, Illia Zabarnyi, 22, lakini wanajua kuwa dili halitawezekana hadi msimu wa joto.

Mshambuliaji wa Chelsea na Ureno Joao Felix, 25, pia anavutiwa na Aston Villa lakini wangeweza tu kuchukua mchezaji mmoja kwa mkopo kutoka Stamford Bridge.

Mshambulizi wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 20, anatarajiwa kuondoka Brighton kwa mkopo kabla ya mwisho wa dirisha la uhamisho.